St.Andrew Parish, Bahari Beach icon

St.Andrew Parish, Bahari Beach APK

2 votes, 5.0/5

The description of St.Andrew Parish, Bahari Beach

Saint Andrew Parish, Bahari Beach App, ni programu mahususi ya kuwajuza na kuwawezesha waamini na wanaparokia wote walioko ndani na nje ya mipaka ya parokia kupata taarifa muhimu kuhusu maendeleo ya parokia yao. Muumini atapata taarifa rasimi za parokia yake kadiri zinavyotolewa na uongozi wa Parokia.

St. Andrew Parish, Bahari Beach App inakuwezesha kutembelea na kuperuzi taarifa nyingi za Parokia ya Mtakatifu Andrea Mtume, Bahari Beach kupitia Website ya Parokia. Pia St. Andrew Parish, Bahari Beach App itakuwezesha kuzijua kikamilifu taarifa zingine zinazojili katika Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, T.E.C., na Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki.

St. Andrew Parish, Bahari Beach App inakuwezesha na kukupa ufahamu mkubwa wa namna unavyoweza kushiriki katika maendeleo ya parokia yako kwa kwa kutoa Katekesi juu ya Utoaji wa Kumtolea Mungu, maana ya Zaka na Sadaka. Mwenyezi Mungu anakubariki kwa namna nyingi je, unawezaje kumshukuru Mungu.

St. Andrew Parish, Bahari Beach App wajumbe mbalimbali wa Halmashauri Walei na Kamati zao wanaweza kujua tarehe ya ushiriki wao katika mikutano husika kulingana na vitengo vyao. Pia taarifa muhimu za parokia zinazotolewa kupitia matangazo ya kila Dominika kama vile zamu za Usafi kwa kila Jumuiya Ndogondogo yaani JNNK, mikutano ya JNNK, Michango ya maendeleo ya Parokia, ratiba ya Misa katika JNNK na Parokiani, maadhimisho ya masakramenti na kadhalika. Taarifa hizi zinaweza kupatakina mahali popote na kwa mtu yeyote mwenye simu yoyote aina ya smartphone jamii ya Androids na hali kadhalika Iphones,na pia kupitia Tablets na Ipads punde anapojisajiri katika mtandao wa St. Andrew Parish, Bahari Beach App.

Tunadhamiria na kweli tumekusudia kuendelea kuboresha huduma zetu. Tunakaribisha mirejesho kutoka kwako wa namna St. Andrew Parish, Bahari Beach App inavyoweza kuwakaribu na waamini na jinsi ya kuwapeleka watu kwa Mungu. Usisite kutoa mapendekezo yako na maoni yako ambayo tutayafanyia kazi kwa upendo na shukrani.

Show More
Popular Apps In Last 24 Hours
Download
APKPure App